Saudi Arabia kuanzisha mahusiano upya na Syria
24 Machi 2023Matangazo
Taarifa hii ni kulingana na vyanzo vitatu vyenye uelewa na suala hilo. Hatua hiyo inatarajiwa kuifungulia milango Damascus kurejea kwenye muungano wa mataifa ya Kiarabu.
Kasi ya mawasiliano kati ya Riyadh na Damascus imeongezeka baada ya makubaliano ya kihistoria ya kuanzisha upya ushirikiano kati ya Saudi Arabia na Iran, ambayo ni mshirika mkubwa wa rais Bashar al-Assad, kimesema chanzo chenye mafungamano na Damascus.
Soma pia: Assad azilaumu Uturuki,Saudia,na Qatar
Syria ilikuwa imetengwa na mataifa mengi ya Kiarabu na ya magharibi tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe vilipoanza nchini humo mwaka 2011.