SANTIAGO:Jenerali mstaafu wa Chile Hugo Sala Wenzel kufungwa maisha
29 Agosti 2007Mahakama kuu ya Chile imetoa hukumu yake ya kwanza ya kifungo cha maisha dhidi ya jenerani mstaafu Hugo Sala Wenzel aliyekuwa mkuu wa shirika la kijasusi la Chile CNI wakati wa utawala wa Pinochet.
Hukumu hiyo ndiyo kali kabisa kuwahi kutolewa na mahakama ya Chile dhidi ya maafisa walioshtakiwa kwa makosa ya kukiuka haki za binadamu katika utawala wa Dikteta Augusto Pinochet kuanzia mwaka 1973 hadi mwaka 1990 ambapo takriban watu 3000 waliuwawa au kutoweka..
Shirika la kijasusi la CNI likiongozwa wakati huo na Hugo Salas lilituhumiwa kuwakandamiza wapinzani wa serikali na kuwauwa vijana mnamo mwaka wa 1987 katika kile kilichojulikana kama Opresheni Albania.
Opresheni Albania ni hatua ya kulipiza kisasi iliyochukuliwa na mawakala wa CNI baada ya jaribio la kumuua Pinochet mwaka 1986.
Pinochet alikufa mwaka uliopita kufuatia ugonjwa wa moyo akiwa na umri wa miaka 91.