SANTIAGO: Dikteta wa zamani wa Chile mgonjwa mahtuti
4 Desemba 2006Matangazo
Dikteta wa zamani wa Chile,Augusto Pinochet amepewa kaida za mwisho na padri wa Kikatoliki. Pinochet,alie na miaka 91 alipelekwa hospitali ya kijeshi mjini Santiago,baada kupata mshtuko wa moyo.Madaktari wamesema hali yake imedhibitiwa lakini yungali mgonjwa mahtuti.Pinochet ameshtumiwa mauaji na utekaji nyara wa wapinzani wake wa kisiasa,wakati wa utawala wake wa kidikteta.Lakini,hakuweza kufikishwa mahakamani kwa sababu ya hali mbaya ya siha.Kama watu 3,000 ama waliuawa au walipotea na wengine 28,000 waliteswa wakati wa utawala wa miaka 17 wa jemadari huyo wa zamani.