SANTA MARIA: Wazee wa mahakama kuamua iwapo Jackson ana hatia au la
4 Juni 2005Matangazo
Baraza la wazee wa mahakama,katika kesi ya muimbaji mashuhuri,Michael Jackson nchini Marekani,limeanza kufikiria hukumu ya kutolewa. Baada ya miezi minne ya kutolewa ushahidi,baraza hilo lenye wanawake 8 na wanaume 4 litaamua iwapo Jackson ana hatia au la.Jackson,anakabiliwa na mashtaka 10 ikiwa ni pamoja na mashtaka kuwa mnamo mwaka 2003 alimtendea vibaya mtoto wa kiume.Iwapo atakutikana na hatia,basi muimbaji huyo anaweza kukabiliwa na kifungo cha hadi miaka 18 jelani.Mwanasheria wake amesema,Jackson hana hatia.Baraza la wazee wa mahakama litakutana tena siku ya jumatatu.