1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Santa Maria, Califonia. Kesi ya Michael Jackson sasa kujadiliwa na wazee wa baraza na kutolewa hukumu hivi karibuni.

4 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF7S

Wazee wa baraza katika kesi ya kuwadhalilisha watoto inayomkabili mwanamuziki maarufu Michael Jackson wamepata maelekezo yao ya mwisho na wameanza kuijadili hukumu yao. Baada ya miezi mitatu ya kutoa ushahidi, watoa hukumu hao 12 wanatakiwa kuamua iwapo Jackson ana hatia ya kumshawishi mtoto aliyekuwa chini ya umri na kumpa pombe katika ranchi yake ya Neverland miaka miwili iliyopita. Mwimbaji huyo mashuhuri wa mitindo ya Pop anashitakiwa katika mahakama mjini Santa Maria, califonia katika mashtaka 10. Iwapo atapatikana na hatia , Jackson anakabiliwa na hukumu ya kifungo cha miaka 20 jela.