1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaTunisia

Saied atarajiwa kushinda tena uchaguzi wa urais Tunisia

7 Oktoba 2024

Rais wa Tunisia Kais Saied anatarajiwa kushinda uchaguzi wa urais nchini humo kwa asilimia 89.2 ya kura licha ya idadi ndogo ya watu waliojitokeza kupiga kura.

https://p.dw.com/p/4lTCG
Tunisia | Wakimbizi | Rais Kais Saied
Rais wa Tunisia Kais Saied Picha: Chokri Mahjoub/ZUMA Wire/IMAGO

Hayo ni kulingana na matokeo ya awali yaliyotangazwa na runinga ya kitaifa baada ya kufungwa kwa vituo vya kupigia kura.

Saied mwenye umri wa miaka 66, anatarajiwa kupata ushindi wa kishindo na kuwabwaga wapinzani wake – Ayachi Zammel ambaye yuko gerezani na Zouhair Maghzaoui.

Soma pia: Mgombea urais Tunisia ahukumiwa miaka 12 jela

Miaka mitatu baada ya Saied kujilimbikizia madaraka makubwa, makundi ya kutetea haki za binadamu yanahofia kuwa kuchaguliwa tena kwake kutazidi kuimarisha utawala wake nchini Tunisia.

Tume ya uchaguzi ISIE imefahamisha kuwa takriban watu milioni 9.7 walikuwa na haki ya kupiga kura katika nchi hiyo yenye idadi jumla ya watu milioni 12.