SADC yakubali kupeleka vikosi mashariki mwa DRC
8 Mei 2023Matangazo
Hatua hiyo ni katika juhudi za kusaidia kumaliza machafuko katika eneo hilo.
Tangazo kutoka kwenye mkutano wa kilele wa jumuiya hiyo yenye nchi 16 wanachama, limesema viongozi wanaokutana nchini Namibia wameunga mkono kupelekwa kwa wanajeshi wa kurejesha amani na utulivu mashariki mwa Kongo.
Hata hivyo tangazo hilo halikubainisha idadi ya wanajeshi watakaopelekwa, wala muda wa kuwasili kwao.
Kwa muda wa miongo kadhaa, makundi ya waasi yenye silaha yamekuwa yakiwasumbua raia wa mashariki mwa Kongo.
Jumuiya ya Afrika Mashariki inao maelfu kadhaa ya wanajeshi katika eneo hilo linalopakana na Uganda na Rwanda.