1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiAfrika

Rwanda yasaini makubaliano ya uchimbaji lithium na Rio Tinto

30 Januari 2024

Rwanda imesaini makubaliano na kampuni kubwa ya madini ya Australia Rio Tinto kwa ajili ya utafutaji na uchimbaji madini ya lithium katika taifa hilo la Afrika Mashariki.

https://p.dw.com/p/4bolY
Kigali, Rwanda | Rais Paul Kagame
Rais wa Rwanda Paul KagamePicha: Trinidad Express Newspaper/AFP

Yamina Karitanyi, Afisa Mkuu Mtendaji wa kampuni ya Rwanda ya madini, mafuta na gesi inayomilikiwa na serikali, ametangaza kuhusu hati ya makubaliano katika taarifa ya pamoja, akisema muafaka huo unadhihirisha juhudi za serikali kuimarisha na kuifanya kuwa ya kisasa sekta ya madini nchini Rwanda.

Lawrence Dechambenoit, mkuu wa masuala ya nje katika kampuni ya Rio Tinto amesema wana furaha kushirikiana na serikali ya Rwandakatika kutumia uzoefu wao wa kimataifa ili kuharakisha utafutaji wa madini ya lithium katika mkoa wa magharibi mwa Rwanda.

Soma pia:Uhusiano kati ya Rwanda na Burundi unayumba zaidi

Lithium ni madini muhimu katika utengenezaji wa betri zinazotumika katika magari ya umeme, pamoja na simu za smartphone na vifaa vingine vya elektroniki.