1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaRwanda

Rwanda kuadhimisha Jumapili miaka 30 ya mauaji ya kimbari

6 Aprili 2024

Rwanda inajiandaa kuadhimisha hapo kesho miaka 30 tangu kufanyike mauaji ya kimbari dhidi ya jamii ya walio wachache ya watutsi.

https://p.dw.com/p/4eUgA
Kumbukumbu ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda ya mwaka 1994
Picha ya mwaka 2004 ikimuonyesha rais wa Rwanda Paul Kagame akiwa na huzuni alipotembelea kaburi la jumla huko Gisozi.Picha: Sayyid Azim/AP Photo/picture alliance

Maadhimisho hayo yanakumbushia kipindi cha kutisha zaidi katika taifa hilo la Afrika Mashariki ambapo kulingana na Umoja wa Mataifa karibu watu 800,000 waliuawa.

Soma pia: Macron asema Ufaransa ingeweza kusitisha mauaji Rwanda

Hadi leo hii, makaburi ya jumla yanaendelea kugundulika katika nchi hiyo yenye watu karibu milioni 14. Viongozi mbalimbali akiwemo aliyekuwa rais wa Marekani wakati wa mauaji hayo Bill Clinton wanatarajia kuhudhuria maadhimisho hayo.