1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rwanda yaishutumu Kongo kwa kukiuka makubaliano

20 Januari 2023

Rwanda jana imeishutumu Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kwa kuyatupilia mbali makubaliano yaliyolenga kuleta amani katika eneo la mashariki la nchi hiyo linalokabiliwa na mgogoro.

https://p.dw.com/p/4MTTm
Ruanda Treffen zwichen dem Präsidenten Paul Kagame mit dem kongolesischen Präsidenten Felix Tshisekedi
Picha: Präsidentschaft der Demokratischen Republik Kongo

Rwanda imetowa shutuma hizo wakati mvutano kati yake na jirani yake Kongo ukiongezeka.  Kigali imetowa taarifa ikisema kitisho kinaongezeka na kuituhumu Kongo kwamba inataka kujiondowa kwenye makubaliano yaliyofikiwa mjini Luanda nchini Angola na Nairobi. Taarifa hiyo imeilaumu Kongo kwamba inajaribu kuhujumu makubaliano ya kikanda na hatua hiyo inaweza tu kuonekana kuwa ya makusudi ya kuendeleza mgogoro na ukosefu wa usalama. Mnamo siku ya Jumatano waziri wa mambo ya nje wa Kongo Christophe Lutundula alilituhumu kundi la M23 na serikali ya Rwanda kwamba kwa mara nyingine limeshindwa kutimiza ahadi zao, na kuapa kuwa Kongo itatumia kila njia kuhakikisha usalama wa eneo lake la mashariki.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW