Rwanda yaikosowa Ubelgiji kutomuidhinisha balozi wake
27 Julai 2023Matangazo
Balozi Karega alifukuzwa na serikali ya Kinshasa mwezi Oktoba 2022 kutokana na mvutano kati ya nchi hizo mbili, na ndipo alipoteuliwa kuwa balozi nchini Ubelgiji.
Msemaji wa serikali ya Rwanda, Yolande Makolo, amesema inasikitisha sana kuona kwamba serikali ya Ubelgiji inaonekana imekubali shinikizo la Kongo na propaganda kutoka kwa mashirika na wanaharakati wanaoipinga.
"Hatua hii haifai kwa uhusiano wa mataifa haya mawili," alisema msemaji huyo wa serikali ya Rwanda.
Kongo ilimfukuza Karega ikiishutumu Rwanda kwa kuliunga mkono kundi la waasi wa M23, madai ambayo yamekanushwa na Rwanda.
Wizara ya mambo ya nje ya Ubelgiji bado haijazungumzia suala hilo.