Rwanda kuifadhili Arsenal
28 Mei 2018Matangazo
Ni makubaliano ya miaka mitatu ambayo yataitangaza nchi hiyo kitalii kufuatia idadi kubwa ya wanyamapori inayoongezeka katika mbuga zake kuanzia faru weusi, simba, pundamilia na hata nyani wa milimani. Hata hivyo, mpango huo wa Kagame umekosolewa na wanaohisi kwamba Rwanda ina matatizo mengi yanayostahili kushughulikiwa kuliko nchi hiyo kuingia mkataba na Arsenal, huku wengine wakiifananisha hatua ya rais huyo ya kujiongezea muda madarakani kuwa sawa na Arsene Wenger aliyekuwa meneja wa klabu hiyo ya Arsenal aliyejiuzulu mwaka huu baada ya kuiongoza kilabu hiyo kwa miaka 22. DW imezungumza na mwanauchumi ambaye pia ni mwanaharakati kutoka Tanzania, Mwang'onda Gabriel.