1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiRwanda

RSF yakosoa mazingira ya kifo cha mwanahabari Rwanda

11 Februari 2023

Shirika la Waandishi wa Habari wasio na mipaka RSF limeukosoa mchakato wa kisheria kuhusu kifo cha mwandishi wa habari mashuhuri nchini Rwanda na ambaye alikuwa akiukosoa utawala wa Rais Paul Kagame.

https://p.dw.com/p/4NMVR
Ruanda Journalist John Williams Ntwali
Picha: privat

John Williams Ntwali, aliyekuwa mhariri wa gazeti la The Chronicles, alifariki Januari 18 wakati gari lilipogonga pikipiki aliyokuwa akiendeshwa kama abiria karibu na mji mkuu wa Kigali.

Dereva aliyehusika katika ajali hiyo alikiri kosa na alipatikana na hatia ya "kuua bila kukusudia". Februari 7, alitakiwa kulipa faini ya milioni moja sarafu za Rwanda, ambayo ni sawa na euro 860.

Mada inayohusiana: 

Kipi kilimpata mwandishi aliyefariki, Rwanda?

RSF imebaini kuwa, tangu mwaka 1996, waandishi wa habari wanane wameuawa au kupotea nchini Rwanda, huku wengine 35 wakilazimishwa kwenda uhamishoni. Katika muongo uliopita, vyombo vya habari huru vimepungua na kufungwa na serikali.