Rome. Italia kuwakamata watu wanaohusika na shirika la Ujasusi la Marekani.
25 Juni 2005Jaji mmoja nchini Italia ameamuru kukamatwa kwa watu 13 wanaotuhumiwa kuwa na uhusiano na shirika la ujasusi la Marekani CIA, kwa kuhusika na kumteka nyara mtuhumiwa wa ugaidi kutoka Misr.
Osama Mustafa Hassan alikamatwa katika mitaa ya Milan hapo Februari 2003.
Vyombo vya habari vya Itali vimeripoti kuwa alichukuliwa hadi katika kituo cha jeshi la anga la Marekani katika eneo la Aviano kabla ya kusafirishwa hadi Misr.
Duru za mahakama za Italia zimesema kuwa , akiwa nchini Misr aliteswa wakati wa kuhojiwa. Hivi sasa hajulikani yuko wapi.
Katika siku za nyuma CIA ilikiri kile ilichosema kuwa ni kuwarejesha watuhumiwa wa ugaidi. Hii inamaana kuwa ni kuwapeleka katika nchi zingine kwa siri kwa ajili ya kuwahoji bila ya idhini ya mahakama.