1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ripoti ya Munich yaelezea mkanganyiko wa hali ya usalama

11 Februari 2019

Utaratibu wa kiliberali wa dunia unavunjika,lakini nani anaweza kuunganisha tena vipande vyake? Ni swali linaloulizwa katika ripoti ya kuelekea mkutano wa usalama mjini Munich.

https://p.dw.com/p/3DAJs
Südkorea Grenzanlage zu Nordkorea
Picha: Getty Images/AFP/J. Yeon-je

Dunia imo katika mgogoro - na Marekani tu ndiyo inafanya mambo kuwa mabaya zaidi. Hiyo ndiyo hukumu ya kijasiri ya Ripoti ya Usalama ya Munich (MSR), iliyotolewa Jumatatu kuelekea mkutano wa usalama wa Munich wiki hii, ambao ni mkusanyiko wa kila mwaka wa wawakilishi wa ngazi ya juu wa mataifa makubwa. Makamo wa rais wa Marekani Mike Pence, waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov, na kansela Angela Merkel watakuwa miongoni mwa mawaziri 100 kutoka duniani wanaotarajiwa kujadili ongezeko la ukosefu wa utulivu duniani.

"Enzi mpya ya mashindano ya mataifa makubwa inaanza kujitokeza kati ya Marekani, China na Urusi, ikiambatana na ombwe fulani la uongozi katika kile kilichokuja kujulikana sasa kama utaratibu wa kiliberali wa dunia," aliandika mkuu wa mkutano huo Wolfgang Ischinger, veterani wa diplomasia na balozi wa zamani wa Ujerumani nchini Marekani, katika dibaji yake.

Angalau moja ya chanzo kikuu cha ukosefu huu wa utulivu kiko wazi. Utawala wa Rais Donald Trump mjini Washington unaonyesha kuguswa kidogo tu na kuheshimu makubaliano ya kimataifa, na tweet zake mara kadhaa zinahoji wazi uhalali wa taasisi zikiwemo NATO na Umoja wa Mataifa. Mbaya zaidi: Chini ya Trump, Marekani inaonekana kuwa tayari kuachana na jukumu lake la kiongozi katika kile kinachoendelea kuitwa "ulimwengu huru."

Katika mkutano wa habari siku ya Jumatatu, Ischinger alipata shida kutaja "habari njema kwanza": kwamba licha ya "alama nyingi za kuuliza" kuhusiana na uhusiano wa mataifa ya kanda ya atlantiki, aliichukulia kuwa "ishara kubwa isiyo ya kawaida", kwamba mara mbili au tatu zaidi ya wabunge wa Marekani wanatarajiwa kuhudhuria mkutano wa mwaka huu. Hasa alikaribisha uwepo wa spika wa baraza la wawakilishi Nancy Pelosi na mgombea wa w zamani wa urais Mitt Romney.

Deutschland München Pk Wolfgang Ischinger
Mwenyekiti wa Mkutano wa Usalama wa Munich Wolfgang Ischinger akizindua ripoti ya usalama wa dunia Jumatatu kuelekea mkutano wa usalama mjini Munich wiki hii.Picha: picture-alliance/dpa/K. Nietfeld

'Shauku inayokera kwa madikteta'

Katika nafasi yake, MSR inamtuhumu Trump kwa kuonyesha "shauku inayochukiza kwa watawala wa kibabe duniani, hii ikiashiria kuwa utawala huu unaishi katika dunia ya 'baada ya haki za binadamu." Hii, inahoji ripoti, inadhoofisha juhudi za Marekani kuongoza mataifa ya kiugawana ya dunia kujenga utaratibu mpya wa kiliberali," kama alivyosema waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo mwezi Desemba, na kupinga mataifa makubwa ya kidikteta. "Kwa washirika wa kanda ya Atlantik w amuda mrefu, ni vigumu bado kuvumilia wakati Trump akiwasifu viongozi wa kiliberali kuanzia Brazil hadi Ufilipino," alisema ripoti hiyo.

"Nyaraka za kimkakati za Marekani zimezinyooshea vidole China na Urusi kama wapinzani muhimu zaidi," ripoti hiyo inaendelea, lakini uhasama kati ya mataifa hayo makubwa unajitokeza kwa njia tofauti. Mgogor kati ya Washington na Beijing umejikita hasa kwenye masuala ya uchumi na biashara, kwa mfano, huku Urusi na China zikijiona kama muungano dhidi ya mataifa ya magharibi, hata wakati zikibakia kwenye ushindani wa kikanda baina yao.

Uhasama kati ya Marekani na Urusi, wakati huo, unaendelea kutwama kwenye tuhuma kuhusu silaha, na MSR inatoa matumaini kidogo kwamba hali hii itaboreka katika muda wa karibuni. Baada ya kufutwa kwa mkataba wa udhibiti wa silaha za nyuklia za masafa ya kati INF, hatua nyingine za udhibiti wa silaha zinaweza pia kukabuiliwa na kitisho, inaonya ripoti hiyo. "Inaonekana hakuna uwezekano kwamba watarefusha mkataba mpya wa START unaohusu silaha za kimkakati za nyuklia zaidi ya 2021, wakati ambapo muda wake utaisha," ilisema ripoti hiyo.

Umoja wa Ulaya 'haujajiandaa'

Na vipi kuhusu Ulaya, ambayo inaonekana kutoa mchango unaozidi kuw amdogo kimkakati katika yote haya? Umoja wa Ulaya hasa hauna maandalizi ya kutosha kwa ajili ya enzi mpya ya mashindano ya mataifa makubwa," imetangaza MSR, jambo linalobainishwa na mjadala mpya kuhusu "uhuru wa kimkakati" wa Ulaya. Kunaonekana kutokuwa na mpango mbadala wa namna Ulaya inaweza kujikwamua katika sera yake ya kimataifa ya usalama.

Vietnam APEC-Gipfel | russischer Präsident Wladimir Putin und US-Präsident Donald Trump
Rais wa Marekani Donald Trump (kulia) na mwenzake wa Urusi Vlamdir Putin (kushoto). Mizozo kati ya mataifa hayo makubwa inatishia mustakabali wa utaratibu wa kiliberali, inasema ripoti ya usalama ya Munich.Picha: picture-alliance/AP Photo/J. Silva

Siku ya Jumatatu, Ischinger aliwaambia maripota kwamba "2019 utakuwa mwaka wa maamuzi kuhusu hatma ya Umoja wa Ulaya," kwa sababu ya uchaguzi wa bunge la Ulaya mwezi Mei na uteuzi wa rais mpya wa benki kuu ya Ulaya mwezi Oktoba. Kwa sababu hiyo ilikuwa muhimu, kwamba Mkutano wa Usalama wa Munich MSC mwaka huu unawaonyesha washiriki wasiotoka Ulaya kwamba Umoja wa Ulaya uko tayari kupigaia maslahi yake kwa kujiamini."

Kwa ujumla, ripoti inahitimishakwamba dunia inapweleza kwenye "kipindi kipya," ambamo walinzi waliosalia wa maadili ya kiliberali wanajaribu wawezavyo kuongoza dunia kupita kwenye kipindi cha mashaka na ukosefu wa utulivu. Maoni ya MSR yanashtua: "Baadhi ya wagombea kwa ajili ya jukumu lililoongezeka kama wasimamizi wa utaratibu wa kiliberali wana nia lakini hawana uwezo, wengine wana uwezo wa wastani lakini hawako tayari au hawawezi kutumia uwezo wao."

'Brexit yaifanya ya UK kutotabirika'

Athari moja ya kipindi hikicha mpito ni kwamba kinaweza kuwa na fursa kwa mataifa yalioko kwenye nafasi ya pili kama Canada, Japan na Uingereza. Wakati Uingereza ilitoa mchango muhimu katika ujenzi wa utaratibu wa kiliberali baada ya vita, na, kama mwanachama wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, bado ushawishi kwenye siasa za kikanda, madhara yasiotabirika ya kuondokakatika Umoja wa Ulaya yameiweka nchi hiyo kwenye mwelekeo mpya.

"Kilichokuwa wazi hata hivyo, ni kwamba Brexit itaendelea kusababisha majeraha kwa pande zote kwa miaka mingi ijayo," inasema ripoti hiyo, licha ya upinzani wa mara kwa mara kutoka London, Paris na Berlin kwamba mataifa hayo bado yataendelea kushirikiana.

Muungano wa waumini wa makubaliano ya pande nyingi?

Hivyo nani amebakia kukusanya vipande vya utaratibu unaosambaratika? Ischinger aliulizwa swali kama hilo Jumatatu: "Nani atachukuwa jukubu hilo? Je, kuna mataifa yanayochukuwa jukumu? Je, Umoja wa Ulaya unaweza kubeba dhamana, au ni dhaifu sana? Na ikiwa ni dhaifu sana, nani mwingine atafanya hivyo? Au tuliache tu litokee: kwamba utaratibu wa kimataifa wa kiliberali, wenye msingi wake katika taasisi, kanuni na sheria, uvunjike vipande vipande? Kwa maslahi ya Ujerumani na Ulaya,  hilo litakuwa tukio lamaafa.

Deutschland Berlin Bundestag Angela Merkel und Heiko Maas
Kansela Angela Merkel na waziri wake wa mambo ya nje Heiko Maas, wanakubaliana juu ya haja ya kuundwa muungano wa mataifa yanayoamini katika utaratibu wa makubaliano ya pande nyingi.Picha: picture-alliance/dpa/M. Kappeler

Katika ujumbe wa karibunikwa njia ya video kabla ya kuhudhuria mkutano huo, kansela Angela Merkel alisema alitaka kufanya kuendeleza taasisi hizo za kimataifa. Hili sasa, alisema, ni "muhimu kama ilivyokuwa wakati wa vita baridi."

Alisisitiza kuwa Ujerumani bado inasimama nyuma ya utaratibu w akiliberali wa dunia, hisia zilizoungwa mkono na waziri wake wa mambo ya nje Heiko Maas, ambaye hivi karibuni alitoa wito wa kuundwa kwa "muungano wa kimataifa wa waumini wa makubaliano ya pande tofauti." Ingawa ugumu wa kufanikisha hilo unoanekana tayari katika mgogoro wa sasa wa Ujerumani na mshirika wake wa karibu zaidi Ufaransa, kuhusiana na mradi wa ujnezi wa bomba la gesi la Nord Stream 2.

Zaidi ya hayo, utafiti mpya uliofanywa na Wakfu wa Ujerumani wa Friedrich Ebert uligundua kwamba ni asilimia 42tu ya raia wa Ufaransa ndiyo wanaamini nchi yao inapaswa kuendelea kutoegemea upande kwenye masuala ya kimataifa, ikiliganishwa na asilimia 59 ya Wajerumani. Vivyo hivyo, Wajerumani wengi zaidi kuliko Wafaransa wanakataa uingiliaji wa kijeshi (asilimia 65 kwa asilimia 50), jambo linaloakisiwa katika tamaduni tofauti za kisiasa mjini Berlin na Paris.

"Mgogoro wasasa wa ushirikiano wa kanda ya Atlantik ni changamoto kubwa zaidi kwa Ujerumani kuliko ilivyo kwa Ufaransa, ambayo mara zote imefuata mkondo huru zaidi," inahitmisha MSR.

Lakini inaendelea kuwa na mashaka namna ya hasa tofauti hizi zinaweza kuondolewa. Haionekani kwamba kutakuwa na hatua kubwa kwenye mkutano wa Munich wiki hii, ingawa: Siku chache zilizopita, rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alifuta ghafla ushiriki wake, akizongwea na matatizo ya kisiasa nyumbani.

Mwandishi: Iddi Ssessanga/dw

Mhariri: Josephat Charo