1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBrazil

Ripoti: Nusu ya mataifa ya kidemokrasia duniani yanashuka

30 Novemba 2022

Shirika la IDEA limesema katika ripoti yake iliyotolewa hii leo, kwamba nusu ya mataifa ya kidemokrasia duniani yanashuhudia mmomonyoko wa demokrasia, hali hii ikichochewa na vita nchini Ukraine na mzozo wa kiuchumi.

https://p.dw.com/p/4KHvs
Thailand APEC 2022 Gipfel in Bangkok - Proteste
Picha: Chalinee Thirasupa/REUTERS

Shirika la kimataifa la utafiti wa sera la International IDEA limesema katika ripoti yake iliyotolewa hii leo, kwamba nusu ya mataifa ya kidemokrasia duniani yanashuhudia mmomonyoko wa demokrasia, hali hii ikichochewa na vita nchini Ukraine na mzozo wa kiuchumi.

Ripoti hiyo imesema idadi ya mataifa ya kidemokrasia yalio na mmomonyoko mbaya zaidi wa demokrasia, ambayo yanaihusisha Marekani tangu mwaka uliyopita, imeongezeka kutoka sita mwaka 2020 kwa kujumuisha El Salvador kwenye orodha hiyo.

Mengine ni Brazil, Hungary, India, Mauritius na Poland. Katibu Mkuu wa International IDEA Kevin Casas-Zambora, ameitaja Marekani hasa kuwa inayotia wasiwasi mkubwa.

Kati ya mataifa 173 yalioangaziwa na ripoti ya International IDEA, 104 yalikuwa ya kidemokrasia na 52 kati yake yalikuwa yanashuka.

-