Riek Machar apinga mazungumzo ya Nairobi
21 Juni 2024Matangazo
Kiongozi huyo amedai kuwa rasimu mpya ya makubaliano hayo inalenga kudhoofisha makubaliano ya awali ya amani.
Machar alimwandikia mpatanishi kwenye mazungumzo hayo na kupinga rasimu ambayo anasema inalenga kuanzisha uongozi mwingine utakaochukua nafasi au kushirikiana na ule ulioanzishwa kutokana na makubaliano ya amani yaliyosainiwa mwaka 2018.
Soma zaidi: Salva Kiir adai mataifa ya Magharibi yanataka kuuchelewesha uchaguzi nchini mwake
Kiongozi huyo wa zamani wa waasi alitia saini makubaliano na Rais Salva Kiir ambayo yaliweza kusitisha vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka mitano na kusababisha vifo vya watu karibu 400,000, huku mamilioni ya wengine wakiyahama makazi yao.