1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Real Madrid dhidi ya Manchester City zimetoka sare ya 1-1

10 Mei 2023

Katika mechi ya kwanza ya nusu fainali ya kuwania kikombe cha klabu bingwa barani Ulaya Champions League Real Madrid dhidi ya Manchester City zimetoka sare ya moja kwa moja.

https://p.dw.com/p/4R7MT
Champions League Halbfinale Real Madrid Manchester City
Picha: Ruben Albarran/IMAGO

Katika kandanda, michezo ya duru ya kwanza ya nusu fainali ya kuwania kikombe cha klabu bingwa barani Ulaya Champions League imefungua pazia usiku wa kuamkia leo kwa mtanange wa kukata na shoka kati ya Real Madrid dhidi ya Manchester City.

Katika mchano huo ambao ulikuwa wa vuta nikuvute magwiji hao wa skoa wamelazimishana kutoka sare ya moja kwa moja. Kwa nyakati tofauti washambuliaji Vinícius Júnior na  inícius Kevin de Bruyne waliwainua mashabiki wao kwa mikwaju ya mbali. Goli la utangulizi kwa upande wa Madrid liliwekwa kimiani na Vinicius lakini katika nusu ya pili ya mvhezo huo De Bruyne akasawazisha. Duru ya pili itachezwa juma lijalo mjini Manchester.

Manchester City ilionekana kuidhibiti mchezo

Champions League Halbfinale Real Madrid Manchester City
Mchezaji Kevin De Bruyne wa Manchester City Picha: Lagencia/IMAGO

Manchester City ilionekana kuidhibiti mchezo lakini haikuweza ingawa hatua hiyo haikuweza kutoa matunda yoyoyote mchezoni, mchezaji Erling Haaland alipoteza nafasi chache mapema lakini haikuwa kitisho chochote katika muda wote wa mchezo pale katika uwanjia wa Santiago Bernabeu

Nusu fainali nyingine kati ya wataji wa jadi, miamba ya soka la Italia, Inter Milan na AC Milan inachezwa leo.Katika mtanange wa leo timu za Inter Milan na AC Milan zinajiandaa na kile katika lugha ya soka wanakiita "Euroderby."

Rekodi ziunaonesha katika kipindi miaka ya nyuma timu za Italia zilikuwa zikitawala soka la Ulaya. Lakini hii ni nafasi ya kwanza kwa Inter Milan kurejea nusu fainali tangu iliposhinda mataji matatu ya ligi, Kombe la Italia na Ligi ya Mabingwa chini ya mwalimu José Mourinho mwaka 2010.

Soma zaidi:Manchester City yachupa kileleni mwa Ligi Kuu ya Premia

Milan ilishinda mataji yake ya mwisho saba mwaka 2007. Pia ilishinda Ligi ya Mabingwa mwaka 2003, ikisonga mbele dhidi ya Inter kwa mabao ya ugenini katika nusu fainali na kwenda kuwashinda Juventus kwenye mechi ya nusu fainali mwisho.

Chanzo: AP