SiasaAsia
Rasi mpya wa Taiwan aapa kuilinda demokrasia ya kisiwa hicho
20 Mei 2024Matangazo
Rais Lai amesema "nataka kuitolea mwito China kuachana na kitisho chake cha kijeshi na kisiasa dhidi ya Taiwan na kuwa na Jukumu la Kimatifa la kudumisha amani na uthabiti katika ujia wa Bahari wa Taiwan na kuhakikisha dunia ipo huru kutokana na hofu ya vita."
Beijing ambayo awali ilimuelezea Lai kama mtu hatari ilijibu kwa kutoutambua Uhuru wa Taiwan.
Soma pia:Lai Ching-te aapishwa rasmi kuwa rais mpya wa Taiwan
Katika hotuba yake aliyoitoa baada ya kuapishwa, Lai alizungumzia moja kwa moja kitisho cha vita kufuatia miaka mingi ya juhudi za China kutaka kuidhibiti Taiwan, akisema demokrasia ya kisiwa hicho imeimarika na kuwashukuru raia kukataa kuyumbishwa na nguvu za nje na kwa kuitetea demokrasia hiyo.