Rajoelina atangazwa rais wa mpito nchini Madagascar
18 Machi 2009Matangazo
Wakuu wa kijeshi nchini Madagascar wamesema wamemuidhinisha rasmi kiongozi wa upinzani Andry Rajoelina kuwa rais wa kipindi cha mpito nchini humo.
Hatua hiyo imekuja saa chache baada ya rais Marc Ravalomanana kutangaza kujiuzulu na kulikabidhi jeshi madaraka.
Upinzani unamshutumu rais huyo kwa utawala mbaya wa kisiwa hicho.
Zaidi ya watu 100 waliuwawa katika maandamano na ghasia tangu kuanza mzozo huo wa kisiasa mwaka huu.Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki Moon ametoa mwito kwa vyama vyote kubeba jukumu na kurudisha demokrasia nchini humo.
Baraza la usalama na amani la Umoja wa Africa pia limetoa taarifa yake na kugusia juu ya kujiuzulu kwa rais Marc Ravalomanana na kutaka katiba ya nchi hiyo iheshimiwe.
Mwandishi: Saumu Mwasimba/ZR