Rais wa Zimbabwe kupambana na vigogo katika uchaguzi mkuu
22 Juni 2023Viongozi hao watatu tayari wamesajiliwa kugombea nafasi hiyo na tume ya taifa ya uchaguzi, ambayo inatarajia kutangaza orodha ya mwisho ya wagombea waliothibitishwa.
Rais Emmerson Mnangagwa wa chama tawala cha ZANU-PF anawania awamu ya mwisho na anatarajia kupata upinzani mkali kutoka kwa kiongozi wa upinzani Nelson Chamisa, aliyemshinda kwa umbali mdogo katika uchaguzi uliozozaniwa wa mwaka 2018.
Aliyewahi kuwa waziri kwenye serikali ya Robert Mugabe, Saviour Kasukuwere, aliyekimbilia uhamishoni nchini Afrika Kusini baada ya mapinduzi ya mwaka 2017, pia anawania nafasi hiyo, ingawa bado haijulikani kama tayari amerejea nchini humo.
Uchaguzi huu wa Agosti unatarajiwa pia kufuatiliwa kwa karibu, katika taifa hilo lenye historia ya uchaguzi unaogubikwa na machafuko na mivutano.