SiasaUrusi
Rais wa zamani wa Urusi aionya NATO kuhusu vita vya nyuklia
19 Januari 2023Matangazo
Medvedev ambaye anahudumu kama naibu mwenyekiti katika baraza la usalama lenye nguvu la Rais Putin, ameyasema haya kupitia ujumbe aliouandika katika mtandao wa Telegram.
Kiongozi huyo wa zamani aliyehudumu kama rais wa Urusi kati ya mwaka 2008 hadi 2012, amesema jumuiya ya NATO na viongozi wengine wa ulinzi ambao watakutana Ijumaa katika Kambi ya Kijeshi ya Ramstein nchini Ujerumani kujadili mikakati na uungwaji mkono wa juhudi za nchi za Magharibi kuishinda Urusi nchini Ukraine, wanastahili pia kufikiria kuhusiana na athari zitakazotokana na sera yao. Urusi na Marekani ndio wamiliki wakubwa wa zana za nyuklia, wakiwa na asilimia 90 ya zana za nyuklia duniani.