Haki za binadamuVenezuela
Rais Maduro aafiki kufunguliwa tena kwa ofisi ya haki ya UN
24 Aprili 2024Matangazo
Ofisi hiyo ilifungiwa na wafanyakazi wake kuamriwa kuondoka mnamo mwezi Februari mwaka huu.
Maduro aliitoa kauli hiyo akiwa pamoja na Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC, Karim Khan ambaye alikuwa ziarani katika mji mkuu wa Venezuela, Caracas.
Soma pia: Upinzani Venezuela wamsajili mgombea wa uchaguzi wa rais
Mabadiliko hayo ya msimamo yanajiri huku Maduro akikabiliwa na mzozo wa ndani na nje ya nchi kuhusu rekodi ya serikali yake ya mrengo wa kushoto katika masuala ya haki za binaadamu, pamoja na kuukandamiza upinzani wakati akitazamiwa kuwania muhula wa tatu madarakani.