1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ulaya yatolewa wito kuanzisha sera ya pamoja ya ulinzi

21 Januari 2025

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema Ulaya inapaswa kuanzisha sera ya pamoja ya ulinzi na kuwa tayari kuongeza bajeti ya kijeshi kuhakikisha inaweza kujihakikishia usalama wake.

https://p.dw.com/p/4pRPQ
Volodymyr Zelensky
Rais wa Ukraine Volodymyr ZelenskyPicha: Fabrice Coffrini/AFP/Getty Images

Zelensky  amehoji ikiwa kweli rais wa Marekani Donald Trump yuko tayari kuiunga mkono jumuiya ya kujihami ya NATO na usalama wa Ulaya.

Urusi,Ukraine zashambuliana kwa droni usiku kucha

Katika hotuba yake muda mfupi uliopita kwenye jukwaa la kiuchumi la kimataifa huko Davos,Uswizi, Zelensky amekwenda mbali na kuhoji ikiwa kweli Trump atakuwa tayari kuziheshimu taasisi za Umoja wa Ulaya.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW