Rais wa Ujerumani aonya kuhusu"kuwa na taswira ya adui"
24 Desemba 2016Hotuba hiyo ya kawaida ya kila wakati wa sikukuu ya Krismass kutoka kwa rais wa Ujerumani mwaka huu kwa kiasi kikubwa ilihusika zaidi ya tukio la Jumatatu la shambulio la kigaidi katika soko la Krismass mjini Berlin. Watu 12 waliuwawa na wengine 49 walijeruhiwa baada ya anayedaiwa kuwa mshambuliaji Anis Amri kuendesha lori na kuligonga kundi la watu Desemba 19.
"Vifo vingi na majeruhi katika soko la krismass mjini Berlin vimetuogopesha na kuwa kutukera," Rais Joachim gauck alisema katika hotuba iliyorekodiwa kabla na kutangazwa kutoka katika kasri lake katika mji mkuu la Bellevue. "Watu wanajisikia hasira , hofu na kutokuwa na nguvu."
Gauck ameonya kwamba hisia hizi hazipaswi kuruhusiwa kutawala, na kuongeza kwamba hasira haipaswi kugeuzwa kuwa chuki na ghasia. Badala yake , ni juu ya kuwa na umoja na kulinda hali ya kuishi kwa pamoja.
Mtu yeyote ambaye ana hisia, yuko tayari na mwenye kusaidia" anaweza "kubadili hasira na chuki kuwa nguvu ambayo inaweza kuzuwia chuki, ghasia na kuwatendea vibaya wengine," Gauck alisema katika hotuba yake ya mwisho ya Krismass akiwa rais wa Ujerumani.
Mjadala sahihi wa kisiasa
Gauck alionesha wasi wasi katika uwezekano wa jamii kuwa na msimamo mkali - hususan katika mjadala wa kisiasa kuhusiana na sera ya wakimbizi nchini Ujerumani. "Hususan katika wakati wa mashambulizi ya kigaidi, hatupaswi kuongeza kina cha mipasuko katika jamii yetu, ama kuyashuku makundi ama kuelekeza vidole kwa wanasiasa nchini," Gauck alisema.
Hii haina maana , hata hivyo , kwamba mijadala ya kisiasa kuhusiana na sababu na matokeo ya shambulizi yanapaswa kuachwa kando; la hasha, sera za wakimbizi na usalama nchini Ujerumani ni lazima vijadiliwe, lakini kwa kutumia maamuzi sahihi na kuwasikiliza wapinzani wa kisiasa. Kwa Gauck , mchungaji wa zamani , hii inahusiana sana na ujumbe wa kikristo katika krismass. "Hivi sasa, katika siku kama hizi, tunapaswa kukumbuka maana ya krismass na vipi imekuwa sehemu ya utamaduni wetu kupindukia Wakristo."
Kuonesha shukrani
Rais ametoa wito kwa raia wa Ujerumani kuwa na hali ya "kuiamini nchini yao" na kufanya kila linalowezekana kuhakikisha kwamba jamii inabakia "sehemu ya umoja wa mshikamano." "Hata katika wakati huu , wakati nchi ikihangaika na masuala ambayo hayajapatiwa ufumbuzi, " Gauck aliongeza. Hakuelezea "ndoto kubwa," lakini alizungumzia badala yake "kuhusu hali halisi." Gauck alisema anaendelea kukutana na watu ambao wanaifanya Ujerumani kuwa mahali pazuri zaidi pa "kuishi" - iwapo ni kwa kufanyakazi , starehe, katika familia ama kwa kujitolea. "Watu hawa mara zote wamenifanya niweze kujiamini zadi kama rais," alisema.
Katika hotuba yake ya kila mwaka ya Krismass, Gauck pia alitoa sifa maalum na shukrani kwa wauguzi na watoa huduma, waalimu wa chekechea, waalimu, wanajeshi na maafisa wa kisiasa. Lakini pia kwa "vyama vya wafanyakazi na wafanyabiashara, wafanyakazi wanaotoa huduma kwa jamii na wanaohudumia maeneo mbali mbali, na wote wanaofanya sheria inafanyakazi."
Shukrani pia zilitolewa kwa "watu wengi wa kujitolea ambao waliwasaidia wakimbizi na kuonesha kwamba hawapaswi kuachwa bila ya kuhudumiwa na kuwakataa watu kutoka nje ili kulinda maisha yao." Hususan katika nyakati fulani, jamii itakubali "kazi muhimu" za watu hawa. " Sio kwasababu wanafanya kitu ambacho si cha kawaida," Gauck alisema ," lakini ni kwa sababu wanafanya vizuri sana."
Mwandishi : Sabine Kinkartz / ZR / Sekione Kitojo
Mhariri: Zainab Aziz