1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Kais Saied ateua waziri mpya wa mambo ya ndani

Angela Mdungu
18 Machi 2023

Rais wa Tunisia Kais Saied amemtangaza Gavana wa zamani wa mji mkuu Tunis Kamal Feki kuwa waziri wake mpya wa mambo ya ndani muda mfupi baada yaTaoufik Charffedine aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo kujiuzulu

https://p.dw.com/p/4Osgk
ARCHIV | Tunesien | Präsident Kais Saied
Picha: Fethi Belaid/REUTERS

Tangazo hilo limetolewa jana saa chache baada yaTaoufik Charffedine aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo kujiuzulu wakati nchi hiyo ikitawaliwa na ukandamizaji wa wanasiasa wakubwa wa vyama vya upinzani

Soma zaidi Wanaharakati wamkosoa rais wa Tunisia

Awali Feki ambaye ni mfuasi mwaminifu wa Rais Saeid alikataa kuwapa kibali cha maandamano wanachama wa muungano wa upinzani wa Salvation Front  akisema wapo viongozi wanaofanya njama dhidi ya serikali.

Hata hivyo aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani Taoufik Charffedine aliwaruhusu kuandamana. Mwenyewe Charffedine alitangaza kujiuzulu jana kwa sababu za kifamilia.