Rais wa soka wa Uhispania agoma kujiuzulu kwa kosa la busu
25 Agosti 2023Katika mkutano wa dharura wa shirikisho hilo la kandanda uliofanyika siku ya Ijumaa (Agosti 25), Rubiales, mwenye umri wa miaka 46, alisema hatoachia nafasi yake.
Kiongozi huyo wa soka alisema shinikizo alilolipata wiki hii kutoka kwa wanasiasa na vilabu ni jaribio la "kutaka kumuangamiza" na atajitetea kwa kuwachukulia hatua watu hao.
Soma zaidi: FIFA kufungua kesi dhidi ya rais wa shirikisho la soka la Uhispania
Mkuu huyo wa kandanda Uhispania alisema busu lake kwa Hermoso lilikuwa kama kumbusu mtoto na haliwezi kufananishwa na udhalilishaji wa kingono.
Hatua yake ya kuendelea kung'ang'ania uongozi wa shirikisho hilo imewapelekea wanasiasa nchini humo, akiwemo Naibu wa Pili wa Waziri Mkuu, Yolanda Diaz, kutaka serikali ichukue hatua za haraka.