Rais wa Senegal apigia upatu Umoja wa Afrika kujiunga G20
8 Julai 2023Matangazo
Akihutubia kwa njia ya mtandao mkutano wa masuala ya uchumi unaofanyika kwenye mji wa kusini mwa Ufaransa wa Aix-en-Provence, Sall amesema kuukaribisha Umoja wa Afrika ndani ya kundi la G20 utakuwa uamuzi wa kutenda haki iliyocheleweshwa.
Amewambia wajumbe wanaoshiriki mkutano huo kuwa ameridhishwa na hatua inayopigwa kuelekea kuridhia Umoja wa Afrika kujiunga na kundi la G20 akikumbusha kuwa kwa jumla bara hilo linashika nafasi ya nane kwa thamani ya pato ghafi duniani.
Afrika Kusini ndiyo nchi pekee ya Afrika iliyo mwanachama wa kundi la G20 linaloyaleta pamoja mataifa 19 tajiri na yale yanayoinukia pamoja na Umoja wa Ulaya.