SiasaKazakhstan
Rais wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev alivunja bunge
19 Januari 2023Matangazo
Kulingana na taarifa iliyotoka katika afisi yake, Tokayev ameyavunja pia mabunge ya serikali za mitaa nchini humo. Katika ujumbe rais huyo amewaambia raia wa nchi hiyo kwamba anatarajia kuwa uchaguzi huo wa mapema utaleta "mwamko mpya" wa kuiendeleza nchi hiyo iliyo na utajiri wa mali asili, ambayo zamani ilikuwa katika muungano wa Sovieti.
Tokayev alichaguliwa mwezi Novemba baada ya kushinda asilimia 80 ya kura baada ya uchaguzi uliokosolewa kwa ukosefu wa ushindani. Aliahidi kuiunda Pakistan mpya yenye usawa ila changamoto za kiuchumi na mienendo ya kidikteta ndiyo mambo yanayoendelea kushuhudiwa katika utawala wake.