1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Rais wa Iran Ebrahim Raisi kuzikwa leo mjini Mashhad

23 Mei 2024

Rais wa Iran Ebrahim Raisi anatarajiwa kuzikwa leo katika mji mtakatifu Mashhad, siku nne baada kufariki katika ajali ya helikopta pamoja na waziri wake wa mambo ya nje Hossein Amirabdollahian na watu wengine sita.

https://p.dw.com/p/4gC86
Jeneza la rais wa Iran Ebrahim Raisi
Jeneza la rais wa Iran Ebrahim RaisiPicha: Iranian Presidency Office/AP/picture alliance

Rais wa Iran Ebrahim Raisi anatarajiwa kuzikwa leo katika mji mtakatifu Mashhad, siku nne baada kufariki katika ajali ya helikopta pamoja na waziri wake wa mambo ya nje Hossein Amirabdollahian na watu wengine sita.

Jeneza la Raisi lilisafirishwa kwa ndege hadi Mashhad kaskazini mashariki mwa Iran.

Soma pia: Amir wa Qatar, mawaziri wa nje wa Ghuba waenda Iran kumzika Raisi

Mapema leo, maelfu ya raia walitoa heshima zao za mwisho mjini Birjand wakati gari lililobeba mwili wake lilipoendeshwa kupitia barabara za mji huo.

Gwaride la heshima lilisimama kidete wakati ndege iliyobeba jeneza la Rais ilipowasili mjini Mashhad alikozaliwa ambapo atazikwa katika maziara ya imam Reza, eneo takatifu zaidi la Kiislamu nchini Iran na linaloheshimiwa na Waislamu wa madhehebu ya Shia kama eneo la mapumziko la Imam Ali al-Reza wa karne ya 9.