1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Iran asema wataendelea kutoa msaada kwa Hamas

1 Agosti 2024

Rais wa Iran Masoud Pezeshkian amesema watazidi kuimarisha msaada wao kwa kundi la Hamas baada ya kifo cha kiongozi wake Ismail Haniyeh.

https://p.dw.com/p/4j0eY
Rais mpya wa Iran Massud Peseshkian
Rais wa Iran Masoud Pezeshkian amesema watazidi kuimarisha msaada wao kwa kundi la HamasPicha: Iranian Presidency/Anadolu/picture alliance

Pezeshkian alikuwa akizungumza na kiongozi wa ngazi za juu wa Hamas Khalil al-Hayya katika mazungumzo ya simu na kusema Iran haitarudi nyuma hata inchi moja kuunga mkono vuguvugu dhidi ya utawala wa zayuni, huku al-Hayya akiapa kulipiza vikali kifo hicho.

Soma pia: Iran, washirika wake wajadili kisasi cha mauaji ya Haniyeh

Katika hatua nyingine, maafisa wa Iran watakutana na wawakilishi wa washirika wao wa kikanda, kuanzia Hamas wa Palestina, Houthi wa Yemen, Hezbollah wa Lebanon na makundi yaliyopo Iraq ili kukubaliana njia bora ya kujibu shambulizi hilo, duru zenye uelewa wa suala hilo zimesema.

Afisa mwingine mwandamizi wa Iran amesema, kiongozi wa juu nchini humo Ayatollah Ali Khamenei na maafisa wengine wa Kikosi cha Mapinduzi watahudhuria kikao hicho.