Rais wa Iran afariki katika ajali ya helikopta
20 Mei 2024Miili ya viongozi hao pamoja na maafisa wake imepatikana baaada ya saa nzima ya kuwatafuta katika eneo la milima lililokuwa na ukungu mwingi Kaskazini Magharibi mwa Iran.
Shirika la habari la Iran bado hadi sasa halijatoa chanzo cha ajali hiyo.
Ebrahim rais aliyeaga dunia akiwa na miaka 63, amekuwepo madarakani tangu mwaka 2021 wakati Iran ikikumbwa na maadamano makubwa dhidi ya serikali, mgogoro wa kiuchumi uliozidi kuiathiri nchi hiyo hasaa baada ya Marekani kuiwekea vikwazo, pamoja na mvutano uliopo kati yake na adui yake wa muda mrefu Israel.
Soma pia:Rais wa Iran aripotiwa kufa katika ajali ya helikopta
Hapo jana Jumapili kiongozi wa juu wa taifa hilo Ayatollah Ali Khamenei aliwatolea wito raia wa Iran kuwa watulivu na kutokuwa na wasiwasi juu ya uongozi wa Jamhuri hiyo ya kiislamu.
Taarifa zinasema tayari kiongozi wa juu zaidi wa Iran,Khamenei ametangaza siku tano za maombolezo ya kitaifa na amemtangaza Mohammad Mokhber kukaimu nafasi ya rais. Mokhber, aliye na miaka 68, alikuwa makamu wa rais.