1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIndia

Rais wa India azindua bunge jipya baada ya uchaguzi

27 Juni 2024

Rais wa India amezindua bunge jipya siku ya Alhamisi baada ya uchaguzi wa kitaifa na kutaja vipaumbele vya miaka ijayo vya serikali ya Waziri Mkuu Narendra Modi.

https://p.dw.com/p/4hZbp
Draupadi Murmu, rais wa India
Draupadi Murmu, rais wa IndiaPicha: Prakash Singh/AFP/Getty Images

Vipaumbele hivyo ni pamoja na kuongeza kasi ya utekelezaji mageuzi ya kiuchumi na kuimarisha viwanda vidogo na vya kati ili kuibua fursa za ajira.

Rais Draupadi Murmu amesema uchumi wa India umekuwa ukikuwa kwa haraka miongoni mwa mataifa makubwa ulimwenguni kwa wastani wa asilimia 8 katika kipindi cha miaka minne.

Modi alichaguliwa kuongoza hilo lenye idadi kubwa ya watu ulimwenguni kwa awamu ya tatu licha ya chama chake kushindwa kupata wingi wa kutosha bungeni na kutegemea washirika wa chama cha madhehebu ya Kihindu kuongoza taifa hilo kwa miaka mitano.