1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Guinea-Bissau Umaro Sissoco avunja bunge

5 Desemba 2023

Rais wa Guinea-Bissau Umaro Sissoco Embalo amechukua uamuzi wa kulivunja Bunge lililokuwa linatawaliwa na upinzani.

https://p.dw.com/p/4Zmij
Guinea-Bissau | Präsident Umaro Sissoco Embalo trifft führende Militärs
Picha: Privat

Hayo yanajiri baada ya kiongozi huyo kusema tukio la makabiliano ya risasi katika mji mkuu wa Bissau siku ya Ijumaa, lilikuwa ni jaribio la mapinduzi. Taarifa hiyo imeendelea kuwa tarehe ya uchaguzi  ujao wa Bunge itatangazwa baadaye kulingana na sheria za nchi hiyo.Wiki iliyopita, wanajeshi wa ulinzi wa taifa waliwatoa kizuizini bila ya kufuata utaratibuwa kisheria mawaziri wawili waliokuwa wamezuiliwa na polisi kwa tuhuma za rushwa, na kusababisha makabiliano ya risasi na vikosi maalum vya ulinzi wa rais. Jaribio hilo la mapinduzi ni la pili katika eneo la Afrika Magharibi na Kati ndani ya muda wa wiki moja baada ya jaribio lengine lililoshindwa la wiki iliyopita nchini Sierra Leone.