Xi Jingping asema ulimwengu unapitia "changamoto kubwa"
24 Oktoba 2024Rais Xi Jingping wa China amewaambia viongozi katika mkutano wa kilele wa jumuiya ya nchi zinazoinukia kiuchumi ya BRICS, kwamba ulimwengu unakabiliwa na changamoto kubwa na hivyo kundi hilo linabidi kuwa na nguvu ya kuleta uthabiti.
Soma pia: Putin aonya dhidi ya majaribio ya kuishinda Urusi
Kiongozi huyo wa China ametowa mwito huo, ikiwa ni siku ya mwisho ya mkutano huo wa BRICS unaofanyika katika mji wa Urusi wa Kazan. Hotuba yake mbele ya viongozi wenzake wa BRICS pia imetahadharisha kuhusu changamoto zinazoukabili ulimwengu katika amani, huku akitowa mwito wa kusitishwa vita katika Ukanda wa Gaza na kuzuiwa kutanuka kwa vita zaidi nchini Lebanon.
Katika mkutano huo, Rais Masoud Pezeshkian wa Iran ameukosoa Umoja wa Mataifa kwa kutokuwa na uwezo wa kuzima mgogoro huo wa kikanda.