1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Rais Volodymyr Zelensky afanya ziara katika jimbo la Kharkiv

29 Julai 2024

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amefahamisha kwamba ametembelea eneo la mashariki la Kharkiv linalopakana na Urusi leo Jumatatu.

https://p.dw.com/p/4is9S
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akizungumza na waandishi wa habariPicha: Sergei Supinsky/AFP/Getty Images

Jimbo hilo la Kharkiv na mji wa Kharkiv ambao ni mji wa pili kwa ukubwa nchini Ukraine limekuwa likikabiliwa na mashambulizi ya kila siku ya vikosi vya Urusi tangu nchi hiyo ilipovamia Ukraine Februari mwaka 2022.

Soma pia: Ukraine yaendelea kuyalenga maeneo ya Urusi 

Zelensky amesema eneo hilo ni moja ya maeneo yanayokabiliwa na hali ngumu lakini amewaambia wanajeshi wa nchi yake kwenye eneo hilo kwamba Ukraine inawategemea.

Vikosi vya Urusi vimekuwa vikijaribu kuuteka mji mdogo ulioko kilomita tano kutoka eneo lake la mpakani tangu ilipoanzisha operesheni ya kushambulia jimbo hilo la Kharkiv.

 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW