1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Rais Putin azilaumu nchi za Magharibi kuhusu vita Ukraine

21 Februari 2023

Hotuba ya mwaka ya Putin yatowa mwelekeo wa Urusi kuhusu vita nchini Ukraine wakati rais wa Marekani Joe Biden akitarajiwa kuwahutubia washirika wake akiwa Poland baada ya kuitembelea Kiev Jumatatu

https://p.dw.com/p/4Nmad
Putins jährliche Ansprache vor der Bundesversammlung in Moskau
Picha: Sergei Karpukhin/TASS/IMAGO

Rais wa Marekani Joe Biden yuko Poland ambako atafanya mazungumzo na mwenyeji wake rais Andrzej Duda na kukutana pia na viongozi wengine kutafuta uungaji mkono wa Ukraine. Huko Urusi rais Vladmir Putin nae amelihutubia taifa akitowa mwelekeo wa vita vyake nchini Ukraine, kwa kuzilaumu hasa nchi za Magharibi.

Rais wa Marekani Joe Biden aliwasili jana Jumatatu usiku huko Warsaw akitokea Kiev alikofanya ziara ya kuonesha uungaji mkono wa Marekani  katika mapambano ya Ukraine dhidi ya uvamizi na mashambulizi ya Urusi.

Ziara yake ya mjini Kiev ilikuwa ya kushtukiza na  maana yake haikutangazwa mapema  na akiwa huko alionekana akitembea kwenye mitaa ya mji huo mkuu wa Ukraine akiwa bega kwa bega na rais Zelensky.Zelensky: Vikosi vya Urusi vinaendelea kuishambulia Kiev

Ukraine | Krieg | Besuch US Präsident Biden in Kiew
Picha: Evan Vucci/AP Photo/picture alliance

Aliiahidi kwamba Marekani itasimama pamoja na Ukraine kadri inavyohitajika na ahadi hiyo anatarajiwa pia kuitowa akiwa huko Poland anakotazamiwa kuwatishia shime washirika wa Jumuiya ya kujihami ya Nato kusimama zaidi na Ukraine.Katika baadhi ya yale aliyoyazungumza jana huko Kiev alisema  wakati rais Putin wa Urusi alipoanzisha uvamizi wake kiasi mwaka mmoja uliopita, alifikiri Ukraine ni dhaifu na nchi za Magharibi zimegawika, alifikiri atafanikiwa kuyazima mataiafa hayo lakini alikosea.

Na hotuba yake baadae  leo inatarajiwa  kuonesha ni kwa namna gani nchi yake imesaidia kuushawishi ulimwengu kuiunga mkono Ukraine na kusisitiza uungaji mkono wa washirika wa Jumuiya ya kijeshi ya NATO upande wa Ulaya Mashariki.

Kwa upande mwingine huko Urusi rais Vladmir Putin muda mfupi uliopita vile vile ametowa hotuba yake iliyokuwa ikisubiriwa  kwa hamu kubwa, akigusia juu ya mwelekeo wa nchi hiyo katika kile inachokiita operesheni ya kijeshi nchini Ukraine itakayoingia mwaka wake wa pili mwezi huu.

Putins jährliche Ansprache vor der Bundesversammlung in Moskau
Picha: Sergei Karpukhin/TASS/IMAGO

Hotuba ya Putin kwenye bunge la nchi hiyo imetowa tathmini kwa viongozi wa kisiasa na kijeshi kuhusu vita vya Ukraine lakini pia tathmini ya hali ilivyo kimataifa pamoja na kutowa mwelekeo wa hali halisi ya nchi hiyo baada ya nchi za Magharibi kuiwekea vikwazo chungunzima.NATO: Urusi ni tishio la moja kwa moja kwa washirika

Rais Vladmir Putin amesema nchi za Magharibi bado zinaendelea kumimina fedha kuunga mkono vita na nchi hizo zilianza kuifanya Ukraine kuwa mpinzani wa Urusi muda mrefu. Na kwa hivyo amekwenda mbali zaidi kwa kusema nchi hizo zinawajibika kubeba dhamana kikamilifu juu ya vita hivyo.

Mara chungunzima rais huyo wa Urusi amekuwa akitowa sababu za kuhalalisha uvamizi wake nchini Ukraine kwa kuzituhumu nchi za Magharibi kwamba zinaitishia nchi yake. Hii leo pia amerudia hayo hayo akisisitiza kwamba nchi za Magharibi ndizo zilizoanzisha vita hii na Urusi inatumia nguvu kuimaliza vita hiyo na inapambana kurudisha haki ya kihistoria.

BG Musiker, die aus Russland fliehen, finden in Georgien ein neues Publikum
Picha: Maxim Shemetov/REUTERS

"Hatua kwa hatua tutayamaliza matatizo yanayotukabili kwa uangalifu na kwa ustadi.''

Hotuba hiyo ya Putin imeoneshwa moja kwa moja na vituo vyote vya televisheni vya taifa.

Kulikuwa na usalama wa hali ya juu katika eneo la katikati ya mji mkuu Moscow kabla ya hotuba hiyo ya mwaka ya rais Putin iliyogusia pia masuala ya kiuchumi na kijamii iliyotolewa mbele ya bunge la nchi hiyo.

 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW