1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Miaka 50 ya uhusiano wa kibalozi pamoja na Israel

11 Mei 2015

Rais Reuven Rivlin wa Israel amepokelewa rasmi hii leo nchini Ujerumani alikoanza ziara rasmi ya siku 3 kuadhimisha miaka 50 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizi mbili.

https://p.dw.com/p/1FOEP
Rais Joachim Gauck akimpokea kwa heshima za kijeshi rais Reuven Rivlin wa IsraelPicha: Reuters/H. Hanschke

Rais Reuven Rivlin wa Israel amepokelewa rasmi hii leo nchini Ujerumani alikoanza ziara rasmi ya siku 3 kuadhimisha miaka 50 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizi mbili.

Ziara ya rais wa Israel Reuven Rivlin inaanza siku tatu baada ya sherehe za kuadhimisha miaka 70 tangu utawala wa wanazi wa Ujerumani uliposalim amri na kumalizika vita vikuu vya pili vya dunia pamoja na mauwaji ya halaiki ya Holocaust ambapo wayahudi milioni 6 waliuliwa-kisa kilichopelekea kuundwa dola ya Israel mnamo mwaka 1948.

Rais Joachim Gauck alimtandikia zulia jekundu na kumkaribisha kwa hishima zote za kijeshi rais Rivlin katika bustani ya kasri la Bellevue-makaazi rasmi ya rais Gauck.

Kizazi kipya cha Israel chazidi kuvutiwa na Ujerumani

"Ujerumani na Israel zinataka,licha ya tofauti za kisiasa kuimarisha uhusiano wao wa kirafiki na kupambana na dhidi ya hisia za chuki dhidi ya wayahudi na ubaguzi."Wamesisitiza rais Joachim Gauck na mgeni wake,rais Rivlin wa Israel baada ya mazungumzo yao mjini Berlin.Mzozo wa mashariki ya kati nao pia waliuzungumzia huku rais wa shirikisho Joachim Gauck akisisitiza umuhimu wa kuishi kwa amani wayahudi na waarabu.Kuhusu kuimarika uhusiano kati ya Israel na Ujerumani,rais Gauck anasema:"Nnafurahi kuona kwamba katika kipindi cha miaka iliyopita,idadi ya wanaokuja inazidi kuongezeka.Sio tu wanaokuja kwa matembezi,bali pia wanaosalia muda mrefu katika mji huu na hasa kutoka Israel.Kizazi kipya kimeugundua mji wa Berlin.Wote wanaandika na kuzungumzia kuhusu mji huu.Kinachowavutia kuja huku sio kwasababu ya vituo vya maovu yaliyotokea,kinachowavutia zaidi ni hali nzuri ya kuishi pamoja."

Deutschland Joachim Gauck empfängt Reuven Rivlin PK
Picha: Getty Images/AFP/J. MacDougall

Rais Rivlin amepangiwa kuweka shada la mauwa hivi punde katika kiunga nambari 17 cha makumbusho-katika mtaa wa Grunewald-magharibi ya mji mkuu Berlin ambako maelfu ya wayahudi walisafirishwa kwa reli hadi katika kambi za mateso-wakati wa utawala wa wanazi.

Ufumbuzi wa mzozo wa mashariki ya kati mazungumzoni

Kesho rais Reuven Rivlin atakutana na kansela Angela Merkel na waziri wa mambo ya nchi za nje Franck Walter Steinmeier.Mazungumzo yao yatatuwama katika suala la kuundwa serikali mpya ya muungano ya mrengo wa kulia iliyoundwa wiki iliyopita nchini Israel pamoja pia na mustakbal wa utaratibu wa amani pamoja na wapalastina."Nchini Ujerumsani tunahisi ufumbuzi wa madola mawili ndio njia pekee ya kupatikana amani ya kudumu katika eneo la Mashariki ya kati" amesema kansela Angela Merkel mjini Berlin hii leo.

Deutschland Israel Regierungskonsultationen Merkel
Kansela Angela Merkel akiongoza kikao cha pamoja cha serikali ya Ujerumani na Isreal mjini Bonn May nane mwaka huuPicha: picture-alliance/dpa/R. Jensen

Rais wa Israel atakamilisha ziara yake jumatano ijayo kwa kuutembelea mji wa kaskazini wa Kiel.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/dpa

Mhariri: Iddi Ssessanga