1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Putin wa Urusi aonekana mara ya kwanza tangu uasi wa Wagner

26 Juni 2023

Rais Vladmir Putin wa Urusi kwa mara ya kwanza tangu ulipotokea uasi wa kundi la wapiganaji la Wagner, ameonekana kupitia video akiwa kwenye ikulu ya Kremlin, akihutubia mkutano wa jukwaa la vijana

https://p.dw.com/p/4T4sN
Russland | TV Ansprache Putin
Picha: via REUTERS

Rais Vladmir Putin wa Urusi kwa mara ya kwanza tangu ulipotokea uasi wa kundi la wapiganaji la Wagner, ameonekana kupitia video akiwa kwenye ikulu ya Kremlin, akihutubia mkutano wa jukwaa la vijana, uliopewa jina la ''wahandisi wa baadae''.

Kwenye hotuba hiyo ameyasifu makampuni kwa kuhakikisha uendeshaji imara wa sekta ya viwanda nchini humo katika wakati ambapo Urusi inakabiliwa na changamoto nyingi kutoka nje.

Lakini wakati huohuo rais Putin pia inaelezwa amefanya mazungumzo na rais wa Iran, Ebrahim Raisi kwa njia ya simu leo Jumatatu ambapo kiongozi huyo wa Iran amezungumzia uungaji mkono wake kwa utawala wa Urusi kuhusiana na tukio la Juni 24.

Rais Putin amezungumza pia na mtawala wa Qatar Sheikh Tamim Bin Hamad al Thani ambaye pia ameonesha kumuunga mkono.