1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Putin anasema vikosi vya nyuklia 'daima' viko macho

9 Mei 2024

Rais Vladimir Putin wa Urusi amesisitiza kwamba nchi yake itafanya kila liwezekanalo ili dunia isitumbukie kwenye vita lakini amesema kuwa Urusi haitakubali vitisho kutoka upande wowote.

https://p.dw.com/p/4fgAH
Rais Vladimir Putin wa Urusi
Rais Vladimir Putin wa UrusiPicha: Ramil Sitdikov/Tass/IMAGO

Kauli hiyo ameitoa katika hotuba yake ya kuadhimisha "Siku ya Ushindi" wa umoja wa kisovieti dhidi ya manazi wa Ujerumani katika vita vikuu vya pili.

"Urusi itafanya kila linalowezekana kuzuia mzozo wa kimataifa. Lakini wakati huohuo hatutaruhusu mtu yeyote kututishia. Nguvu zetu za kimkakati ziko tayari kila wakati." Alisema Putin katika hotuba yake.

Viongozi watano wa nchi zilizokuwa zamani kwenye umoja wa kisovieti walihudhuria sherehe hizo. Viongozi hao ni kutoka nchi za Belarus, Kazakhstan, Kyrgyzstan, Tajikistan na Turkmenistan.

Soma pia:Vladmir Putin: Urusi haitaruhusu vitisho

Viongozi wengine washirika wa Urusi waliohudhuria  ni kutoka Cuba, Laos na Guinea-Bissau.

Hotuba ya Siku ya Ushindi ya Putin inatolewa wakati wanajeshi wake wanasonga mbele nchini Ukraine na mara tu baada ya kula kiapo cha kuongoza muhula wa tano madarakani.