1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Rais Vladimir Putin aitolea msharti Ukraine ili amalize vita

14 Juni 2024

Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema nchi yake itamaliza vita vyake dhidi ya Ukraine ikiwa nchi hiyo itakubali kuacha matarajio yake ya kujiunga na Jumuiya ya Kujihami ya NATO na kukabidhi majimbo manne inayoyadhibiti.

https://p.dw.com/p/4h38U
Rais Vladimiri Putin alipozuru Uzbekistan
Rais Vladimir Putin wa Urusi ameitolea msharti Ukraine ili amalize vita nchini humoPicha: Mikhail Metzel/REUTERS

Kyiv imekataa masharti ya Moscow na imepinga kujisalimisha. Haya yanajiri kabla ya mkutano wa nchini Uswisi ambao Urusi haikualikwa.

Putin ameweka masharti hayo ya upeo wa juu kudhihirisha imani kwamba majeshi yake yana uwezo zaidi katika vita dhidi ya Ukraine.

Amesema ikiwa Ukraine itakataa kama hapo awali, basi watalibeba jukumu la kisiasa na kimaadili kutokana na kuendelea kwa umwagaji damu na kuongeza kuwa masharti kwa ajili ya kuanza mazungumzo yatakuwa tofauti. 

Mshauri wa rais wa Ukraine Mykhailo Podolyak ameyataja masharti ya Putin ni sawa na kupendekeza kwamba Ukraine ikubali kushindwa na kutia saini uhuru wake.