1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Putin ampandisha cheo afisa wa ngazi za juu wa magereza

20 Februari 2024

Rais Vladimir Putin amempandisha cheo afisa wa ngazi ya juu wa magereza nchini Urusi, siku chache tu baada ya kifo cha kiongozi wa upinzani Alexei Navalny.

https://p.dw.com/p/4cdCM
Urusi |  Alexei Navalny
Alexei Navalny ni kiongozi wa upinzani Urusi na mkoasoaji mkubwa wa Rais Vladimir Putin Picha: Dmitri Lovetsky/AP/picture alliance

Mkurugenzi wa Taasisi ya Kupambana na Rushwa ambayo ilianzishwa na Navalny, Ivan Zhdanov amesema kuwa hatua hii ya Putin inadhihirisha wazi kuwa ni malipo ya wazi kwa kuwa mtu huyo ambaye amesema alihusika na vitendo vya mateso dhidi ya Navalny alipokuwa gerezani.

Urusi yakataa uchunguzi wa kimataifa kuhusu kifo cha Navalny

Mama mzazi wa mkosoaji huyo aliyefariki siku ya Ijumaa Bi Lyudmila amemtaka Rais Putin kuruhusu kuachiliwa kwa mwili wa Navalny ili aweze kumzika kwa heshima. Ikulu ya Kremlin imekuwa ikisema kuwa uchunguzi unaendelea kubaini sababu za kifo hicho.