1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUrusi

Rais Putin ameongeza ukubwa wa jeshi lake

17 Septemba 2024

Rais wa Urusi Vladimir Putin ameongeza ukubwa wa jeshi la nchi hiyo, hii ikiwa ni mara ya tatu tangu ilipoiavamia kikamilifu Ukraine, Februari, 2022.

https://p.dw.com/p/4khB7
Rais wa Urusi Vladimir Putin
Rais Vladimir Putin amesema analenga kuongeza ukubwa wa jeshi lake, katikati ya vita vinavyozidi kati ya Urusi na UkrainePicha: Vyacheslav Prokofyev/picture alliance

Kulingana na amri ya Rais iliyotolewa mapema leo, Urusi inalenga kufikisha idadi jumla ya wanajeshi 2,389,000, na wanaotakiwa kuongezwa ni milioni 1.5.

Mwezi Disemba, Putin aliongeza ukubwa wa jeshi lake na kufikia milioni 2.2, huku wanajeshi wakiwa milioni 1.33.

Lengo hili jipya linaongeza ukubwa wa jeshi kwa asilimia 50, ikilinganishwa na karibu milioni moja, mwanzoni mwa vita vyake na Ukraine.