Rais Mubarak atangaza kutowania tena urais
2 Februari 2011Hata hivyo kauli yake hiyo haitoshi kuwatuliza mamia kwa maelfu ya watu wanaondamana katika mji mkuu Cairo na miji mingine kwa siku ya nane sasa.
Rais Barack Obama wa Marekani akizungumza mara baada ya hotuba ya Rais Mubarak, amesema mabadiliko nchini Misri yanatakiwa kuanza mara moja.Hata hivyo makundi ya upinzani nchini Misri yamesema hayatajadiliana na Rais Mubarak na wamemtaka ajiuzulu.
Mohamed ElBaradei mtu ambaye baadhi wanamchukulia kuwa ni kiongozi wa vuguvugu hilo la umma, amesema siku ya Ijumaa ijayo imepewa jina kuwa ni siku ya kuondoka kwa Rais Mubarak.
Wakati huo huo serikali kadhaa za nje zimewahamisha raia wake kutoka Misri, huku Ujerumani ikizidisha onyo kwa raia wake wanaotaka kwenda Misri, likiwemo eneo la mapumziko la ufukwe wa Red Sea ambalo ni maarufu sana kwa watalii wa kijerumani.
Mwandishi:Aboubakary Liongo/ZPR
Mhariri:Oummielkher