SiasaSri Lanka
Rais mteule wa Sri Lanka aahidi mabadiliko ya kiuchumi
23 Septemba 2024Matangazo
Dissanayake amesema hayo baada ya kupata ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi uliogubikwa na hasira za wapigakura dhidi ya hali ngumu ya uchumi.
Dissanayaka wa chama JVP mwenye umri wa miaka 55, amempiku mshindani wake wa karibu kwa zaidi ya kura milioni 1.3 na ameapishwa Jumatatu asubuhi akimrithi Rais Ranil Wickremesinghe aliyechukuwa madaraka baada ya mapinduzi ya umma ya mwaka 2022 yaliyouangusha utawala wa Rais Gotabaya Rajapaksa.
Rais huyo mpya wa Sri Lanka anakabiliwa na kibarua kigumu cha ukarabati uchumi wa nchi hiyo uliodorora pamoja na kufanikisha mpango wa uokozi wa mabilioni ya dola kutoka shirika la fedha la kimataifa IMF.
Viongozi wa India, Pakistan, China na visiwa vya Maldives wamempongeza Dissanayake kwa ushindi wake.