Macron akabiliwa na shinikizo la kumtangaza waziri mkuu mpya
27 Agosti 2024Rais Emmanuel Macron bado ameshindwa kupata waziri mkuu mkuu mpya, kumaliza mkwamo wa kisiasa unaoikabili Ufaransa. Kufuatia hatua hiyo kiongozi wa chama cha mtazamo mkali wa siasa za mrengo wa kushoto nchini humo cha LFI, Jean Luc Melenchon ametowa mwito wa kufanyika mchakato wa kumuondowa madarakani kwa kura ya kutokuwa na imani nae. Jana Jumatatu rais Macron alikataa fikra ya kutangaza serikali ya mrengo wa kushoto ili kumaliza mkwamo wa kisiasa,hatua iliyozusha hasira miongoni mwa wanaouunga mkono muungano wa siasa za mrengo wa shoto nchini Ufaransa.Macron amesema kutangaza seriikali ya mrengo wa kushoto ni kuhatarisha uthabiti wa kitaasisi. Kiongozi wa chama cha kijani Marine Tondelier ameitaja kauli hiyo ya rais Macron kuwa fedheha akisema kiongozi huyo anaapuuza matokeo ya uchaguzi.