1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBrazil

Maeneo zaidi ya jamii za wazawa kuanzishwa Brazil

29 Aprili 2023

Rais wa Brazil Luiz Inácio Lula da Silva ametia saini amri za kuanzisha maeneo zaidi yaliyohifadhiwa kwa ajili ya jamii za wazawa kwenye taifa hilo la Amerika ya Kusini

https://p.dw.com/p/4Qhpk
 Lula decrees six new Indigenous reserves
Picha: Carl de Souza/AFP

Uamuzi huo ambao ni kwanza kufanyika tangu mwaka 2018 unalenga kutenga maeneo mapya sita ya jamii za wazawa ambao wengi bado wanaishi kwenye vijiji vilivyo misituni.

Akionesha dhamira ya kutimiza ahadi yake ya kuzuia ukataji wa miti na uharibifu mkubwa wa mazingira hususani kwenye msitu wa Amazon, rais Lula amesema ataendelea kutenga ardhi kwa ajili ya jamii za asili, zinazosifika kwa utunzaji mkubwa wa mazingria.

Mwanasiasa huyo wa mrengo wa kushoto anataka ifakapo mwaka 2030 kusiwe na shughuli zozote za ukataji wa miti ndani ya msitu wa Amazon, unaotegemewa na Ikolojia ya dunia.