1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ramaphosa: Afrika hailazimishwi kuchukua upande duniani

21 Agosti 2023

Rais Cyril Ramaphosa amesema Afrika Kusini haiwezi kulazimishwa kuchukuwa upande wa kuegemea madola makubwa yenye nguvu katika siasa za ulimwengu.

https://p.dw.com/p/4VP5d
 Präsident von Südafrika Cyril Ramaphosa
Picha: Stanislav Krasilnikov/TASS/dpa/picture alliance

Kiongozi huyo pia amesema Mkutano wa kilele wa 15 wa BRICS utajadili masuala kadhaa ikiwemo suala muhimu la uwezekano wa jumuiya hii kutanuka na kuongeza wanachama zaidi, ili juhudi zake zifanikiwe jumuiya ya BRICS inahitaji kujenga ushirikiano na nchi nyingine zenye mtazamo na malengo kama yake. Hatutokubali kuingizwa kwenye mivutano baina ya madola yenye nguvu duniani.Rais huyo wa Afrika Kusini ameyasema hayo jana Jumapili wakati akijiandaa wiki hii kuwakaribisha viongozi wenzake wa kundi la ushirikiano la nchi zinazoinukia kiuchumi, BRICS, utakaofanyika mjini Johannesberg. Ramaphosa amesema nchi yake itasaini makubaliano kadhaa na China.Hatua ya Afrika Kusini ya kuandaa mkutano huo wa kilele imesababisha kumulikwa kwa ushirikiano wake na Urusi, ambayo pia ni mwanachama wa BRICS, na hasa baada ya nchi hiyo ya Afrika Kusini kukataa kulaani uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.Hata hivyo, Rais Vladmir Putin anayetakiwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC hatohudhuria mkutano huo na badala yake atawakilishwa na waziri wake wa mambo ya nje Sergei Lavrov.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW