Rais Biden asitisha kampeni baada ya kugundulika na UVIKO
18 Julai 2024Matangazo
Msemaji wa White House, Karine Jean-Pierre amesema Biden aliyekuwa tayari amepata chanjo dhidi ya virusi vya UVIKO na kadhalika ile ya kuongezewa nguvu alijihisi vibaya baada ya kupata maambukizi hayo.
Hali hiyo ilimfika kiongozi huyo, akiwa kwenye kampeni za uchaguzi huko Nevada. Alikutana na wafuasi mapema Jumatano lakini alikatisha hotuba yake katika jimbo hilo ambalo lina nguvu sawa za ushawishi kati ya chama chake cha Democrats na kile cha Republican.
Hata hivyo Ikulu ya Marekani imesema Biden atarejea katika makazi yake ya kibinafsi huko Delaware ambapo atajitenga huku akiendelea kutekeleza majukumu yake yote kikamilifu wakati huo.