Biden: Marekani haitoitenga Ukraine katika vita na Urusi
8 Machi 2024Matangazo
Katika hotuba yake ya hali ya taifa katika bunge la Marekani, Biden amesema Marekani haitoiacha Ukraine. Zaidi amesema "Ukraine inaweza kuizuia Urusi iwapo tutasimama na Ukraine na kuipa silaha za kujitetea. Hicho tu ndicho Ukraine inachoulizia, hawataki kupelekewa majeshi wa Marekani, isitoshe hakuna majeshi ya Marekani katika vita vya Ukraine na ninadhamiria hali iendelee kuwa hivyo. Ila sasa msaada kwa Ukraine unazuiwa na wale wanaotaka tujiondoe kutoka kwenye uongozi wetu wa dunia."Biden vile vile amelaani kauli zilizotolewa na mtangulizi wake Donald Trump kuhusiana na Jumuiya ya Kujihami ya NATO, ambapo alisema hatotoa msaada wowote kwa nchi wanachama wa NATO iwapo Urusi ingeshambulia mojawapo ya nchi hizo.